ads

adds

DEWJI:MAMBO MAZURI YANAKUJA SIMBA

 Baada ya kutofanya vizuri katika mechi nne mfululizo,mashabiki kuwalaumu viongozi na baadhi yao walisusa kwenda uwanjani katika michezo za Mashujaa na Ihefu hatimaye mwekezaji  Mohammed Dewji amesikia kilio chao kuelekea Dabi ya April 20. 


Katika mechi 4 za hivi karibuni Simba imepoteza mwelekeo na kujikuta ikisalia kushindania taji moja tu kati ya matatu iliyokuwa ikiwania awali. Simba  ilitolewa na Al Ahly katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye michezo miwili ya robo fainali,Simba ilipoteza kwa mikwaju ya penati didi ya Mashujaa kwenye mchezo wa CRDB Confederation cup na kutolewa katika michuano hiyo. Mchezo wa ligi kuu dhidi ya ihefu ulimalizika kwa sare  bao 1-1 

Msimamo wa ligi kuu unaongozwa na Yanga wenye alama 55 ,Azam FC wakiwa na alama 50 na nafasi ya tatu ni Simba wenye alama 46 tofauti ya alama 9 dhidi ya Yanga wanaoongoza ligi. Ili Simba aweze kusalia katika mbio za  kutwaa Ubingwa anapaswa kushinda mechi zote zilizosalia ikiwemo Dabi ya tarehe 20 dhidi ya Yanga.

Mwekezaji wa Simba bado anamatuamaini na ubingwa wa ligi kuu hivyo leo tarehe 15 April zikiwa zimesalia siku tano pekee kuelekea Dabi amewaita viongozi mbali mbali na kuzungumza nao. baada ya kikao amenukuliwa akisema

"Nimefanya kikao na viongozi wa Simba kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua,Kikao kimeenda vizuri wanasimba tusife moyo tuendelee kushirikiana"





Post a Comment

0 Comments