KAGERE AHARIBU SHUGHULI YA YANGA AKIICHARAZA COASTAL UNION

 Klabu ya Simba imegoma kabisa kuwaachia Yanga ubingwa wa msimu huu baada ya kulazimisha ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union mchezo uliopigwa dimba la Mkwakwani jijini Tanga.Benard Morrison alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Wagosi wa  kaya dakika ya 39 kipindi cha kwanza lakini Coastal Union wakasawazisha kupitia Patrick dakika ya 76. Shukrani za kipekee zimwendee super sub MK14 "meddie kagere" aliyebadili matokeo kwa kufunga goli safi dakika ya 90+3 ya mchezo huo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kuwa na pointi 40 kwenye michezo 18 waliyocheza msimu huu wakipishan alama 11 na Yanga yenye pointi 51 wakicheza michezo 19. Yanga na Simba zitavaana mwishoni mwa mwezi April tarehe 30 na mchezo huo utakuwa mgumu sana kwa pande zote mbili na unaweza kuamua bingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Kama Simba angepoteza mechi hiyo basi Yanga wangekuwa kileleni kwa pointi 14 zaidi na wangeshaanza kujiandaa kusherekea ubingwa wa ligi kuu lakini mambo bado kabisa.

Coastal Union wao wanabaki nafasi ya 12 wakiwa na pointi 21 baada ya michezo 19 ya ligi. Kama wangeshinda mechi na simba wangefikish pointi 24 na kuwa nafasi ya 8.

Post a Comment

1 Comments

  1. Merkur 15c Safety Razor - Barber Pole - Deccasino
    Merkur poormansguidetocasinogambling 15C Safety Razor https://deccasino.com/review/merit-casino/ - Merkur - 15C for Barber Pole is apr casino the perfect introduction to the herzamanindir.com/ Merkur Safety https://octcasino.com/ Razor.

    ReplyDelete