ads

adds

ZAHERA AGOMA KUONDOKA YANGA BAADA YA KUTIMULIWA

Klabu ya Yanga hapo jana ilitangaza kuachana na kocha wake mkongo Mwinyi Zahera kwa madai ya mwenendo mbovu wa timu hiyo. 




Klabu hiyo ilifanya mkutano na waandishi wa habari ndipo mwenyekiti wa timu hiyo Dr.Msolla alipotoa taarifa ya kumfuta kazi kocha huyo na nafasi yake kuchukuliwa na Charles Boniface Mkwasa. Baada ya tukio hilo AMOSPOTI ilifanya utaratibu wa kukutana na Kocha huyo na kuzungumza naye 

amospoti : Hivi leo mwenyekiti wa klabu Mshindo Msola ametangaza kuachana na benchi zima la ufundi ambalo linaongozwa na wewe je umekubaliana na taarifa hizi?

Zahera : Unapoachishwa kazi mahali popote ni lazima upewe barua maalumu na kwa leo sijapata barua yoyote kutoka Yanga hata kama wametangaza hadharani ule si utaratibu, Sheria inasema ni lazima nipewe barua . Kwa sasa siwezi kuzungumza chochote mpaka pale ntakapopata barua ntawaita wanahabari na kufanya mkutano wa kwamba mimi na Yanga tumefika mwisho.

Amospoti : Lakini wewe ulikuwa ndani ya klabu na umetoka mazoezini leo bila shaka fununu za wewe kuondolewa ,je haukuona uelekeo huu sio wenyewe.

Zahera : Hakukuwa na dalili za mimi kufukuzwa , Tungoje nipate barua ili niweze kusimulia kila kinachoendelea na hata kabla ya kusafiri kwenda Misri nilizungumza na mwenyekiti na kila kitu kilikuwa sawa na akanihakikishia matokeo yoyote ya misri eidha kushinda au kufugwa hawawezi kunitoa na kama kanitoa basi kuna sababu na hiyo sababu itaonyeshwa kwenye barua.

Amospoti : Je wakikupa barua inayoonyesha umefukuzwa utachukua hatua gani?

Zahera :Mi sina tatizo na ntakubaliana nao kwani wao ndio mabosi kinachosubiriwa ni barua na waniandikie sababu za kunifuta kazi nami ntakujibu maswali yote.

Amospoti : Lakini walikupa tageti kwamba lengo lao ni kuingia hatua ya makundi kombe la shirikisho au Ligi ya Mabingwa

Zahera :Hakuna mtu yeyote aliyenipangia kufika makundi na hata mkataba wangu haujasema hivyo.

Amospoti : Laini wao wamesema walisajili wachezaji kwa ajili ya ushindani na si kwa ajili ya ligi kuu  pekee ila wewe unasema kwa ajili ya ligi?

Zahera : (anacheka kidogo) Kesho nikipata barua ntajibu maswali yote mliyonayo na hapo mtajua ukweli 

Amospoti : Je utaondoka au utabaki? na vipi kuhusu fedha unazodai?

Zahera : Mimi nilikuwa na mkataba na hata wewe unajua mtu yeyote aliye na mkataba anapaswa kudai pesa  kama unavunja mkataba . Na kuhusu mshahara niliokuwa nalipwa au silipwi utajua ntakapopata barua na kufanya mkutano na vyombo vya habari.

Amospoti : Wakati wanatangaza hivi na Barua hawajakupa tayari wamekwishakiuka masharti ya mkataba je utadai fidia juu ya hili au kuwashtaki?

Zahera : Hapana siwezi washtaki , mkataba upo na wao wanauheshimu na wanasababu maalumu ya kunifukuza hivyo nasubiri barua kutoka kwao.

Kwa majibu hayo ya Zahera ni dhahili Kocha Zahera bado hajaondoka rsmi klabuni hapo na majibu kamili tutawaletea hivi karibuni



Post a Comment

0 Comments