ambapo kama akishinda viporo vyote atakuwa sawa na Simba mwenye pointi 22 akicheza michezo 9 kushinda 7 sare 1 kufungwa 1. Tukumbuke Mkwasa amechukua timu ikiwa na Pointi 7 na ameikuta timu iliyo kamili, Wachezaji wa Yanga walisajiliwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera hivyo jambo lolote jema likitendeka basi Zahera anastahili sifa au lawama.
Nimekuwekea chambuzi iliyochambuliwa na wanaYanga mara baada ya kushinda mchezo wake dhidi ya Ndanda na mchezo huo ukiongozwa na Kocha wa muda Boniface Charles Mkwasa.
Mchambuzi wa Yanga
1.yanga nyingine,mambo yaleyale ya zahera .mabadiliko pekee ni utulivu wa timu kiuchezaji kwa siku 2 za mazoezi ,mkwasa angalau kajitahidi kuonyesha kitu japo uwanja ulikua changamoto kwa'plan'yake
2:Tshishimbi🙌pale/vile ndivyo anavyostahili kucheza.uimara wake kama kiungo mkabaji uliwapa utulivu sana mabeki .
3:nimemuelewa sana jafari mohammend 🙌hakuwa bora sana kupandisha timu lakini alifanya jukumu lake la msingi kwenye kukaba .
4:molinga!kitu pekee cha 'maana kwa timu'alichokifanya ni kukubali kuuacha ule mpira kwa sibomana .He's good kwenye kumiliki mpira lakini kwa viungo wa yanga wanahitaji straika mwenye kasi,nguvu pale mbele
5:sibomana patrick 🙌alikuwa na uchu sana wa mechi .unaweza kuona 'attempt'zake na jinsi alivyotamani kupiga ile faulo.
6:Ally sonso ni mlinzi mzuri wa kati.ananguvu na timing nzuri kwenye kuwin mpira kwa mastraika .nilitegemea mkwasa amuondoe pembeni .
7:ndanda walikuwa na mastraika watatu wenye kasi lakini walikosa kiungo mwenye jicho la kutoa pasi za mwisho kwenye mikimbio yao.
8:Paulo maona:akiwa na mpira kama mtoto aliye pakwa asali mdomoni .unatamani angecheza katkati na sio beki
9:Juma abdul 🙌beki mwandamizi aliye amua maamuzi magumu kwaajili ya timu
Ni wachezaji wenye uzoefu pekee ndio wanaoweza kuwa na udhubutu ule.
Ni wachezaji wenye uzoefu pekee ndio wanaoweza kuwa na udhubutu ule.
10:balama mapinduzi🙌 So far anabaki kuwa mchezaji active kwenye kikosi cha yanga ,msimu huu .
Swali la amosoti.com ni je Wachambuzi kaliba hii wataendelea kuwepo siku Yanga ikifungwa?
0 Comments