ads

adds

WACHEZAJI WALIONUSULIKA NA PANGA LA MKWASA HAWA HAPA

Klabu ya Yanga inajiandaa kufanya usajili wa nguvu msiu huu wa dirisha dogo lililofunguliwa tarehe 15 Novemba na litafungwa tarehe 15 Disemba ,Baadhi ya wachezaji wataondolewa 


huku wengine wataendelea kubaki klabuni hapo, inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga unaweza ukawabakisha wachezaji Farouk Shikalo, Lamine Moro na Papy Tshishimbi ndani ya kikosi chao katika msimu huu wa dirisha dogo.

Orodha hiyo inatajwa kutokana na kumshawishi Kaimu Kocha, Boniface Mkwasa juu ya kiwango chao walichoonesha ndani ya timu.

Mbali na hao, wengine waliotajwa ni  Juma Balinya, Patrick Sibomana, Sadney Urikobh na David Molinga.

Molinga ambaye amekuwa akitupiwa lawama kadhaa juu ya kukosa umakini langoni, naye anatajwa kama sehemu ya wachezaji watakaobaki ndani ya kikosi cha Yanga.

Post a Comment

0 Comments