ads

adds

UJUMBE WA ARSENAL KWA GRANIT XHAKA

Kiungo wa Arsenal Granit Xhaka ameendelea kupata masaibu mazito klabuni hapo  mara baada ya kuvua jezi ya Arsenal mbele ya  mashabiki ya kutolewa nje


Mchezaji huyo alitoa lugha ya matusi kwa mashabiki wa Arsenal baada ya kutolewa nje kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace .

Mchezaji huyo alivuliwa unahodha wa timu hiyo na hajacheza mchezo wowote wa timu yake tangu tukio hilo litokee na kocha wa timu hiyo amethibitisha mchezaji huyo kutomtumia kwenye mchezo dhidi ya Leicester City.

Kocha wa timu hiyo Unai Emery amethibitisha nyota huyo anaweza kuondoka mwezi  january na kunauwezekano asicheze mechi yoyote ndani ya Arsenal mpaka msimu wa dirisha dogo utakapofunguliwa. Unai amenukuliwa 

"Sidhani kama ataweza kucheza tena,kama yuko radhi kuitetea jei ya Arsenal basi ni jambo jema , mchezaji huyo anafahamu alipokosea na anaonekana kujutia hivyo ni vyema tukawa karibu naye zaid .Kama yuko vizuri kwa asilimia 100 kuisaidia timu hilo ni jambo zuri zaidi"





Post a Comment

0 Comments