Klabu ya Yanga ilitangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kwa utendaji mmbovu. Mara baada ya kumfukuza AMOSPOTI ilifanya utaratibu wa kusikia
maoni ya kocha huyo ndipo sintofahamu ikaibuka na kuacha maswali ya nani wa kumuamini kati ya Dr Msolla -Mwenyekiti Yanga na Kocha Mwinyi Zahera ?
Swali hilo limetokana na mapokeo na majibu ya Zahera. Nimenukuu maneno ya Mwenyekiti wa Yanga Dr Msolla
DR.Msolla alisema
"Leo tumefikia maamuzi kama kamati ya utendaji ya kuachana na benchi lote la ufundi la klabu ya Yanga , maana yake tumeachana salama na mwalimu mwinyi zahera, mwalimu msaidizi Noel Mwandila na benchi lote la ufundi kuanzia meneja mpaka mlinzi na tumeamua tuanze upya ama mtu atarudi basi atarudi kulingana na utamaduni mwingine lakini sio leo. Tulikuwa na kikao na walimu tumepitia mikataba na kukubaliana nao na tunamalizia taratibu za kumalizana salama hilo ni la muhimu zaii kwa leo, mengine ni mechi na Ndanda siku ya ijumaa na timu itaondoka kesho alfajiri"
Dr Msola alisema amekutana na Kocha Mwiyi Zahera na wamekubaliana kusitisha mkataba. Upande wa Zahera umekanusha taarifa hizo na anadai hajafanya mazungumzo yoyote na uongzozi wa juu na nimemnukuu aliposema
Mwinyi Zahera
" Unapoachishwa kazi mahali popote ni lazima upewe barua maalumu na kwa leo sijapata barua yoyote kutoka Yanga hata kama wametangaza hadharani ule si utaratibu, Sheria inasema ni lazima nipewe barua . Kwa sasa siwezi kuzungumza chochote mpaka pale ntakapopata barua ntawaita wanahabari na kufanya mkutano wa kwamba mimi na Yanga tumefika mwisho.
Kwa maelezo haya ya Zahera ni dhahiri kabisa Yanga wamekurupuka kumfuta kocha huyo kazi na kwa maelezo yake ni wazi kabisa Msola na jopo lake wanawaongopea watanzania.
0 Comments