Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger anajiandaa kupata ofa ya kuwa kocha wa Bayern Munich mpaka mwisho wa msimu (Sun)
Kiungo wa Bayer Leverkusen Kai Havertz yuko tayari kuondoka kutoka Bundesliga.Mchezaji huyo mwenye miaka 20 anatolewa macho na Manchester United.(Marca, via Metro)
Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer imesema kuwa kunaweza kuwa na usajili wa wachezaji wawili , lakini klabu yake itatekeleza kazi hiyo zaidi katika kipindi cha majira ya joto. (Evening Standard)
Chelsea inasikilizia timu zitakazomuwania mshambuliaji Olivier Giroud, 33, na winga Pedro, wakati beki wa kushoto Marcos Alonso akipambana kuhusu kuendelea kubaki Stamford Bridge. (Telegraph)
Fenerbahce inataka kumsajili Pendro kwa uhamisho wa bure majira yajayo ya joto.(Takvim, via Mail)
Pedro pia macho yake kayaangazia China (El Dorsal - in Spanish)
Kiungo wa Manchester United Namanja Matic, 31, yuko tayari kuondoka mwezi Januari. (Manchester Evening News)
Chelsea si lazima kufanya usajili mwezi Januari hata kama marufuku ya usajili itaondolewa, amesema kocha Frank Lampard.(Talksport)
Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland, 19, ana mpango wa kuhamia ligi ya primia katika maisha yake ya soka, anasema baba yake. Alf-Inge Haaland. (Talksport)
Inter na AC Milan wako kwenye mazungumzo kuhusu uwanja mpya wa mpira wenye kugharimu pauni milioni 630 ulio maili nane kutoka San Siro. (Mail)
Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde bado anaungwa mkono na bodi ya klabu lakini kumekuwa na wasiwasi namna timu inavyocheza. (ESPN)
Mlinda mlango wa Sheffield United Dean Henderson, 22, amesema karibu ajiunge na Leeds United kabla ya kujiunga tena na Blades kwa mkopo kutokea Manchester United.(Yorkshire Post)
Zaidi ya 90% ya mashabiki wa Manchester United hawaridhiki na namna klabu inavyoendeshwa, kwa mujibu wa utafiti.(Telegraph)
0 Comments