ads

adds

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 13-11-2019

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kutoa malipo makubwa kuwahi kushuhudiwa ya pauni milioni £340 kwa ajili ya mchezaji wa safu ya mashambulio wa Paris St Germain
mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe. (Le Parisien via Calciomercato)
Cristiano Ronaldo hatalipishwa faini na Juventus kutokana na mienendo aliyoonyesha baada ya kutolewa uwanjani na badala yake kuwekwa mchezaji wa ziada katika mchezo wa pili.
Ingawa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 34, atatarajiwa kuomba msamaha kwa wachezaji wenzake. (Gazzetta dello Sport, in Italian)
Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuomba msamaha
Image captionCristiano Ronaldo anatarajiwa kuomba msamaha
Barcelona wanamtaka mshambuliaji wa timu ya Salzburg mwenye umri wa miaka 19 Erling Braut Haaland kama mtu atakayechukua nafasi ya Luis Suarez mwenye umri wa miaka 32, lakini wanasitasita kuafiki kiwango cha thamani ya mchezaji huyo wa klabu ya Austria cha pauni milioni 85. (ESPN)
Rais wa klabu ya Napoli Aurelio de Laurentiis amepokea Euro milioni 560 kwa ajili ya Ligi ya klabu ya Serie A kutoka Qatar huku mashabiki wakipinga na wachezaji wakigoma . (Mail)
Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United ikiwezekana mwezi JanuariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Tottenham wanatarajia kumchukua mshambuliaji wa kati wa timu ya Roma ya Italia Lorenzo Pellegrini, mwenye umri wa miaka 23, kama mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Christian Eriksen. (Football Italia)
Nemanja Matic anataka kuondoka Manchester United, ikiwezekana mwezi Januari, huku kiungo huyo wa kati Mserbia mwenye umri wa miaka 31 akitarajiwa kwenda Italia. (telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi baada ya Spurs kushindwa na West Ham baada ya kipindi cha mapumziko cha kimataifa. (Telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi
Image captionMeneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akafutwa kazi
Pep Guardiola, ambaye alikuwa kocha wa Bayern Munich kwa misimu mitatu kabla ya kuwasili Manchester City, anaweza kurejea katika Bavaria wakati Niko Kovac anasemekana kuondoka katika timu hiyo. (The Athletic)
Fiorentina wamefanya mazungumzo na meneja wa zamani wa Inter Milan Luciano Spalletti huku wakionyesha kuwa wamemchoka Vincenzo Montella. (Football Italia)
Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim BenzemaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionLyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema
Arsenal wanamfanyia majaribio mchezaji wa safu ya kati wa klabu ya Colorado Rapids Cole Bassett na kijana huyo Mmarekani mwenye umri wa miaka 18 anaweza kujiunga na Gunners mwezi Januari. (Sun)
Wolves wameafiki mkataba wa kumleta kikosini Mholanzi Nigel Lonwijk mwenye umri wa miaka 17 kutoka klabu ya PSV Eindhoven anayecheza katika safu ya kati ifikapo mwezi Januari kwa pauni £170,000. (ED via Birmingham Live)
Lyon wanasaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, mwenye umri wa miaka 31, kumalizia mchezo kule alikouanzia katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Post a Comment

0 Comments