ads

adds

SIMBA YAENDELEA KUWASHA MOTO MKALI NA WABRAZIL WAKE

Kocha Mkuu wa Simba  Bw.Patrick Aussems amesema kuwa wataendelea kujinoa kwa sasa licha ya kuwa na wachezaji wachache ambao wamebaki kwenye kikosi chake.


Aussems amesema kuwa mazoezi kwa wachezaji wake ni muhimu katika kujenga uimara wa kikosi chake kwenye ligi ambayo ina ushindani.

Kocha huyo alinukuliwa akisema "Kuna ushindani mkubwa wa ligi kwa sasa na kila mmoja anapambana kufanya vema, licha ya wachezaji wangu baadhi yao kuitwa timu ya taifa bado tutaendelea na maandalizi.Kuitwa kwao timu ya Taifa ni jambo jema na inamaanisha kwamba kuna kitu ambacho kipo kwao hivyo tutaendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za ligi," 

Miongoni mwa nyota ambao wameitwa kwenye timu za taifa ni pamoja na Miraj Athuman, 'Sheva', Mohamed Hussein 'Tshabalala', Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga hawa wapo timu ya taifa ya Tanzania huku Shiboub akiitwa timu ya Taifa ya Sudan.

Post a Comment

0 Comments