Unaweza kusema Ronaldo ndiye mbabe wa dunia linapokuja suala la kupigania taifa lake la Ureno. Mara zote Ronaldo amekuwa ni jeshi la mtu mmoja kwa Ureno.
Unaweza kumbuka jinsi alivyoiwezesha Ureno kucheza kombe la dunia mwaka 2014 kwa kufunga mabao 4 dhidi ya Sweden kwenye mchezo wa mwisho wa kufuzu na kuibani timu hiyo kwenye mchezo uliomalizika kwa mabao 4-2.
Unaweza pia kumbuka jinsi alivyoipigania timu yake dhidi ya Hispania pale urusi kwa matokeo ya mabao 3-3 huku yote akifunga yeye
na pia utakumbuka alivyofunga mabao 3 muhimu dhidi ya Switzerland kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Ulaya na kuiwezesha timu hiyo kufika fainali na kutwaa ubingwa wa UEFA League.
Ni mengi sana kuyasimulia ila nyota huyo ameendelea kuwatupa mbali wapinzani wake kwa kufunga mabao 98 kwenye michezo 162 aliyoitumikia timu ya Taifa Ureno huku Wayne Rooney aifunga mabao 53,Messi 68,Pelle 77na Zlatan 62.
Nyota huyo anatakiwa kufunga mabao 12 tu ili aweze kuwa mfungaji bora muda wote duniani kwa upande wa timu ya taifa huku anayeongoza kwa ufungaji ni Ali Daei mwenye mabao (109) nafasi ya pili ikichukuliwa na Cristiano Ronaldo mwenye magoli 98 na nafasi ya tatu ni Ferenke Puskas mwenye mabao 84.
0 Comments