advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI 06-11-2019

Real madrid inajiandaa kumtoa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale,30, kwa pauni milioni 70 kubadilishana na mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling ,24.

Chelsea wana mshambuliaji wa Crystal Palace na mchezaji wa timu ya taifa Ivory Coast Wilfred Zaha,26 huku mshambuliaji wa RB Leipzig Tino Werner, 23, akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu wanaowawinda ikiwa marufuku dhidi yao itaondolewa. (Express)
Meneja wa Chelsea Frank Lampard, atakuwa na mpaka pauni milioni 150 kwa ajili ya dirisha dogo la usajili mwezi Januari ikiwa klabu hiyo itaruhusiwa kusajili wachezaji tena baada ya kuzuiwa kufanya hivyo.(Telegraph)
Manchester United na Liverpool wamehusishwa na tetesi za kutaka kumsajili Werner lakini klabu hizi za England zimeieleza RB Leipzig kuwa hazina nia ya kumfanya mshambuliaji huyo kuicha klabu yake.(Mirror)
Manchester United imemfanya kiungo wa pembeni wa West Ham Declan Rice,20, kuwa mchezaji wanayemtolea macho kwa kipindi kijacho cha majira ya joto. Lakini huenda akafikishwa kwenye klabu hiyo mapema mwezi Januari (Goal)
Chelsea imeingia katika kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele,23, huku mchezaji huyo wa zamani wa Celtic macho yake yakiwa Manchester United.(Mail)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho angependa kuifundisha Bayern Munich, kwa mujibu wa kiungo Bastian Schweinsteiger
Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ni miongoni mwa walio kwenye orodha ya Bayern ya kushika nafasi ya Kocha wa zamani Niko Kovac, aliyeondoka kwenye klabu ya mabingwa hao wa Ujerumani.(Guardian)
Manchester United will itabaki bila kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba, 26, kwa karibu majuma mengine manne kwa sababu ya jeraha la kifundo cha mguu. (ESPN)

Wolves wanaandaa ofa ya kitita cha pauni milioni 13 kumnasa kiungo Dejan Kulisevski,23, ambaye pia amehusishwa na klabu za Manchester City na Arsenal.(Sport Witness)
Manchester United imekataa ofa ya pauni milioni 13 kutoka Roma kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Chris Smalling.(Star)
Tottenham imempa ofa mpya mchezaji wa nafasi ya ulinzi Japhet Tanganga, 20, ili kumzuia asiondoke baada ya mkataba wake kukamilika majira yajayo ya joto.(Football Insider)
Wolves imeingia kwenye mbio sambamba na Watford na Newcastle zikimuwinda mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Royal Antwerp, Aurelio Buta 22.(Birmingham Mail)
Leicester imeanzisha mazungumzo na Club Bruges kuhusu uhamisho muhimu wa mshambuliaji Emmanuel Dennis,21, wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Leicester Mercury)
Leicester, Wolves na Everton wanamuwania winga wa Burnley Dwight McNeil, 19.(Teamtalk)
Newcastle na Leicester wanataka kumsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Senegal Habib Diallo,24, kutoka klabu ya Metz ya Ufaransa. (Express)

Post a Comment

0 Comments