Mtendaji mkuu wa ya Simba Senzo Masingisa amezungumzia uvumi wa taarifa zimhusuzo mshambuliaji hatari wa klabu hiyo Kagere huenda akaondoka dirisha dogo lililofunguliwa
hapo jana mpaka disemba 15. Senzo ametowatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwamba timu hiyo bado inamuhitaji sana Kagere na kufuta uvumi wa nyota huyo kuhamia Zamalek ya nchini MisriMazingisa alinukuliwa akisema
“Binafsi siwezi kukubali kumuachia Kagere aondoke hata kwa bilioni moja kwa sababu najua umuhimu wa mchezaji mwenyewe kwetu, sasa unawezaje kukubali kumuachia.
“Unajua yule ni mchezaji muhimu kutokana na mchango wake kwenye timu, lakini pia amekuwa akiburudisha na timu kupata matokeo, sasa leo unaanzaje kukubali kumuachia, si unataka mashabiki waje uwanjani na mabango ya kutaka CEO aondoke.
“Mchezo wa soka ni biashara lakini ambacho unatakiwa kufahamu ni wakati gani ambao unaweza kufanya kitu kwa ajili ya timu na siyo ilimradi kufanya tu kwa kuwa ni kazi.
“Kwa Simba sasa huwezi kumuuza Kagere kwa kuwa ndiye mchezaji muhimu na bora sana na hakuna aliye tayari kuziba pengo lake kwa wakati huu,”
0 Comments