BETI NASI UTAJIRIKE

MANULA AFUNGUKA BAADA YA KUPIGWA CHINI TAIFA STARS


Siku kadhaa zilizopita Kocha wa Taifa Stars Ndayiragije alitangaza kikosi cha Stars ambacho kitacheza mechi za kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Libya na Equatorial Guinea.


Manula ameeleza kuwa kutoitwa timu ya taifa 
haiwezi kumkatisha tamaa kwani ni maamuzi ya kocha pia kocha ndiye anayeona ubora wa mchezaji.

"Naheshimu maamuzi ya kocha na sina tatizo na yeye ,kwa sasa nipo fiti kwa asilimia 100 na nawatakia kila la kheri wachezaji wote ambao wameitwa kwa ajili ya mechi hizo mbili."

Manula amekuwa hana bahati ya kuwa sehemu ya kikosi hicho tangu aitwe mara moja wakati Stars ikiwa na kibarua cha kufuzu CHAN dhidi ya Kenya.


Michezo ya aliyokosekana ni ule wa Rwanda na Sudan na sababu kubwa ilikuwa ni majeruhi. Kilichoshtua mashabiki wa soka ni kutoitwa kwake ilihali amecheza mechi za klabu yake ya Simba kwa kiwango cha hali ya juu.

Kikosi cha wachezaji 27 kiliingia  kambini hapo jana kujiandaa n michezo miwili mikubwa ukiwamo wa kufuzu AFCON dhidi ya Equatrial Guinea na kufuzu kombe la dunia dhidi ya Libya

Post a Comment

0 Comments