advertise with us

ADVERTISE HERE

KOCHA STARS AWAPIGIA MAGOTI WATANZANIA KISA MANULA

Kocha msaidizi wa Timu ya Taifa "Taifa Stars " Mgunda amewaomba msamaha mashabiki wa soka nchini baada ya kutoa kauli ya kumsimanga kipa wa Simba Aishi Manula.Hivi karibuni kocha huyo wa  Taifa Stars alifanya mkutano na wanahabari na alipoulizwa kuhusu manula kukosekana timu ya taif bila ufafanuzi alijibu (namnukuu)

"Hatumchagui mtu kwa sura yake kwa sababu hatukuja kuposa sisi, Tunachagua mchezaji Mtanzania mwenye uwezo wa kucheza"

Kauli hiyo ilimwingiza kwenye utata mkubwa na wapenzi wa soka nchini na kulazimishwa kuwaomba la sivyo siku zake zinahesabika pale Taifa . Mara baada ya malalamiko hayo kocha huyo aliamua kukili kosa lake na kuomba msamaha akidai alinukuliwa vibaya. Kocha Juma Mgunda alisema

"WaTanzania wameninukuu Vibaya.Mimi nilitoa kauli ile kwa Nia nzuri tu nimeshtuka sana Kwani imesambazwa sana wakati mimi nilikuwa na nia nzuri tu.Manula ni Mchezaji wa Tanzania na amefanya makubwa ninacho waomba wa-Tanzania wawe kitu kimoja waje waishangilie Timu yao ya Taifa" 

Taifa Stars inaendelea na mazoezi kuwakabili Equatorial Guinea siku ya ijumaa tarehe 15-11-2019 mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments