ads

adds

IFAHAMU REKODI YA TIMU YA UINGEREZA INAPOTIMIZA MECHI YA 1000 TANGU KUANZISHWA KWAKE

Timu ya taifa la Uingereza leo hii itatimiza mchezo wake wa 1000 tangu kuanzishwa kwake kwenye mhezo wa kufuzu michuano ya ulaya (EURO) mwaka 2020.



Uingereza imekwisha cheza michezo 999 na itafikia mchezo wake wa 1000 dhidi ya Montenegro. Nimekuandalia historia fupi ya timu hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Uingereza imetumia miaka 147 kuwez kuifikia rekodi hiyo ya michezo 1000 na Montenegro itatimiza karne ya pili kucheza na Uingereza baada ya kufanya hivyo mchezo wa 900 zilipokutana 

Hii hapa historia kamili

A. UPANDE WA MECHI

1. Mchezo wake wa kwanza kimataifa ilikuwa dhidi ya Scotland mwaka 1872 Novemba 30 na ulichezwa uwanja wa Hamilton Crescent na ulimalizika kwa sare ya 0-0. Timu ya Montenegro ilicheza na uingereza kwenye mchezo wake wa 900 a matokeo yalikuwa 2-2.

2. Uingereza imeshinda michezo 568 kati ya michezo 999 iliyokwisha cheza.

3. Timu ya Scotland imekutana mara nyingi zaidi na uingereza zikicheza michezo 114. Scotland imefungwa mara 41 na Uingereza ,Huku wales ikifungwa zaidi kwa michezo 67.

4.Mwaka 1882 timu ya Uingereza ilipata ushindi mkubwa zaidi wa mabao 13-0 dhidi ya Ireland. Miaka 17 baadaye waliifunga tena Ireland mabao 13-2.

5. Uingereza imeshawahi kufungwa ugenini mabao 7-1 na timu ya Hungary na imefungwa mabao 7-2 ikiwa uwanja wa nyumbani Wembley dhidi ya Hungary.

B. UPANDE WA WACHEZAJI

1.  Jumla ya wachezaji 1244 wameshaitumikia timu ya taifa Uingereza kwa vipindi tofauti tofauti. wachezaji 9 tu wamefanikiwa kupata jumla ya tuzo 100 za kuitumikia timu hiyo huku wachezaji 356 wakipata heshima hiyo mara moja kwa kila mmoja.

2.Golikipa Peter Shilton amecheza michezo  125 mingi zaidi ya kipa yeyote huku Wayne Rooney akicheza michezo 120 kwa wachezaji ambao wanacheza soka mpaka sasa.

3.Theo Walcott ndiye mchezaji mdogo zaidi kuitumikia uingereza na aliweka rekodi hiyo mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 17 na siku 75. Huku wayne rooney akishikilia rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga na alifanya hiyo akiw na miaka 17 siku 317 dhidi ya Marcedonia.

4. Rooney ndiye mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwa timu ya taifa Uigereza akifunga mabao 53 manne zaidi ya Bob Chalton.

5.Stanley Matthew ndiye mchezaji mzee zaidi kuifungia timu hiyo bao na alifanya hivyo akiwa na miaka 41 na siku 248 na alifanya hivyo Oktoba 1956.

C. UPANDE WA MAKOCHA 

1. Walter winterbolton ndiye kocha wa kwanza muingereza kuiongoza timu hiyo na alikabidhiwa mwaka 1946 na aliiongoza kwa miaka 16.

2. Uingereza imeshawahi kuwa na makocha 19 wa kudumu na Walter Winterbolton akiongoza rekodi ya mechi nyingi zaidi mechi 139.

3.Fabio Cappelo na Sven Glon Erikson ni makocha pekee wasi waingereza kupewa mikoba ya kukinoa kikosi hicho. Na kama utakumbuka fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini basi kikosi kile kiliongozwa na Fabio Capello.

Post a Comment

0 Comments