ads

adds

HUYU HAPA KOCHA MPYA WA YANGA ATAKAYECHUKUA NAFASI YA MKWASA

Klabu ya Yanga imeendelea kumsaka mrithi sahihi wa Mwinyi Zahera na sasa anatajwa Mserbi Nikola Kavazovic aliyewahi ifundisha timu ya taifa Sri Lanka kati ya 2014-2015.



Kocha huyo alishawahi kufundisha vilabu vya Township Rollers ya Botswana (2017-2018), Leopards ya Kenya mwaka 2018 na Klabu ya Free State ya South Afrika msimu huu wa (2018-2019).

Kavazovic anaonekana kulijua vyema soka la Afrika kutokana na uzoefu wake wa kufundisha klabu kadhaa hapa Barani Afrika. Klabu ya Yanga kwa sasa ipo chini ya Charles Boniface Mkwasa "Master" ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa muda na uongozi wa klabu.

Maamuzi ya kumteua Mkwasa yalikuja mara baada ya Kamati tendaji kufikia uamuzi wa kuvunja benchi zima la Ufundi la timu hiyo kutokana na matokeo yasiyoridhisha chini ya Zahera.

Mbali na Kavazovic, Yanga pia ilishawahi kufundishwa na makocha wa Serbia kwa miaka ya hivi karibuni kama Dusan Kondic na Kostadin Papic.

Post a Comment

0 Comments