BETI NASI UTAJIRIKE

HIVI NDIVYO MOHAMMED DEWJI ANAVYOIPELEKA SIMBA KIMATAIFA

Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba Bw.Mohammed Dewji ameendelea kufanya kufuru ndani ya klabu hiyo. Makala iliyopita nilimzungumzia Dewji anavyowapa shida Yanga 




Hasa suala la kiutendaji na mfumo mzima wa klabu ya Simba. Mbele ya Kamera Dewji anasimama kama mwekezaji mkuu wa Simba ila nyuma ya Kamera Dewji anasimama kama Shabiki wa simba mwenye matamanio ya kuona klabu hiyo inafika mbali sana kwenye soka la Afrika . Leo ntakuetea mambo matatu aliyoyafanya Dewji ndani ya Simba ambayo yanaifanya klabu hiyo kuwa ya kipekee kwenye soka la Afrika Mashariki

1. Ujenzi wa kiwanja kwa klabu ya Simba 

Klabu ya Simba ilianzishwa miaka ya 1935 ila mpaka 2019 ilikuwa haina uwanja wake wa mazoezi na mara zote imekuwa ikikodi viwanja mbalimbali vya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi. Kabla Mo hajaichukua timu hiyo aliweka ahadi ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa timu hiyo na leo tunaona Simba ikijiandaa kuupokea uwanja wake wa Bunju na kuanza matumizi. Tukumbuke Mo dewji ameingia Simba mwaka 2017 kama mwekezaji lakini pia ni shabiki kindaki wa timu hiyo hivyo mambo mengi anafanya kwa mapenzi.



2. Kubadili mfumo wa kiutendaji ndani ya Simba 

Tulikwisha zoea vilabu vya Simba na Yanga vikiendeshwa kwa mifumo isiyo na mwelekeo na malengo makuu kwa vilabu hivyo ilikuwa kumfunga mpinzani wake na kutwaa kombe la ligi kuu. Dewji amekuja na mtizamo wa kitofauti kabisa wa kiutendaji. Dewji anataka kuiona Simba ikifanya vizuri kimataifa na si kumfunga mtani na ndio maana amesajili wachezaji wa gharama kubwa ili kujenga kikosi imara na chenye uwezo wa kushindana kimataifa. Sikushangazwa na kujiuzulu kwa mwenyekiti Nkwabi na ukichunguza sana utagundua Nkwabi ni aina ileile ya viongozi wanaowaza kumfunga mtani. Dewji amemleta Senzo Mazingisa kama Afisa Utendaji akiamini kwa uzoefu wa Senzo basi Simba itakuwa ya kimataifa .


3. Uboreshaji wa maslahi kwa wachezaji

Tulikwisha zoea wachezaji wa Simba na Yanga wakiweka kambi Morogoro na Zanzibar na sababu kubwa ya kambi hizo ni kujiandaa kwa mechi ya mtani. Dewji aipoingia tu madarkani alihakikisha wachezaji wote wa Simba wanapata mishahara mizuri,akalipa madeni yote na kabla ya ligi aliwapelika wachezaji hao Afika kusini kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na michuano ya CAF na ligi. kwa upande wa pili hali ni mbaya kwni wnashindwa hata kulipa vyakula mahotelini na kula mlo mmoja wakati mwingine.



Hitimisho: Bado tunarudi palepale kwamba Dewji anawanyoosha Yanga na wanatama Manji achukue timu hiyo hata kwa kuikodi. Mashabiki wa Simba wanaaswa kumwelewa mo kwa namna ya kitofauti na yeye binafsi haoni faida ya kuifunga au kufungwa na Yanga ilihali timu inabaki palepale tangu kuanzishwa kwake



Post a Comment

0 Comments