advertise with us

ADVERTISE HERE

ENGLAND YAWEKA REKODI MPYA IKITIMIZA MECHI YA 1000 KWA KISHINDO

Timu ya Taifa la Uingereza maarufu kama Simba watatu hapo jana usiku imeweka historia mpya kwa kufikisha mechi 1000 tangu kunzishwa kwake na kuifikia kwa kishindo


Uingereza iliikaibisha Montenegro kwenye mchezo wa kufuzu EURO 2020 na kufanikiwa kushinda mchezo huo kwa mabao 7-0. Huku Hat trick ikifungwa na Harry Kane

Rekodi moja wapo ni wachezaji 4 kutoka timu 4 zenye ushindani walifanikiwa kufunga kwenye mechi hiyo . 

Harry Kane kutoka Tottenham aliibuka nyota wa mchezo kwa kufunga mabao 3 dakika ya 18,24 na 37 

Marcos Rashford kutoka Manchester United aliifungia Uingereza bao dakika ya 30 huku Tammy Abraham kutoka Chelsea akifunga bao 1 dakika ya 84 

Na mchezaji kutoka Liverpool Alex-Oxlade Chamberlan akifunga bao la kwanza kabisa kwenye mchezo huo dakika ya  11.

Kwa matokeo hayo Uingereza wanakuwa na uhakika wa kufuzu michuano hiyo wakiwa na pointi 18 kwenye michezo 7 waliyocheza.

Post a Comment

0 Comments