ads

adds

CHAMA AWASHIWA MOTO ,CHANZO CHATAJWA

 Kenny Mwaisabula maarufu kama Mzazi, amefunguka kwa kusema kuwa wachezaji wengi wa kigeni wanafeli kutokana na kuendekeza starehe.


Mwaisabula ameeleza wachezaji wengi kutoka nje ya nchi wamekuwa wakifika nchini wakiwa na viwango vizuri lakini baada ya muda wanapotea kwenye ramani.

Mdau huyo amemtaja mchezaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, kuwa ni moja ya wachezaji ambao kwa sasa hawana makali kama alivyotua wakati anatokea Power Dynamos ya Zambia.

Ameeleza kuwa starehe imemgharimu Chama na sasa hana tena ule umaridadi ndani ya dimba kitu ambacho kimesababisha kiwango chake kuporomoka.

"Chama ninayemfahamu mimi si yule wa Simba aliyekuwa mzuri kwa mwaka jana, wachezaji wengi wa nje wakija Tanzania hawamalizi mwaka mmoja wanapotea dimbani, starehe wanaendekeza zaidi kuliko kazi",

Post a Comment

0 Comments