ads

adds

KOCHA MPYA NA MAMBO MAPYA

Klabu ya Azam FC kwa mara ya kwanza imepata ushindi baada ya kufanya vibya mechi tatu zilizopita. Klabu hiyo imefanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya Biashara. 




Kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Ushindi huo wa kwanza chini ya Mromania Aristica Cioaba tangu arejeshwe unaifanya Azam FC ifikishe pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 14.


Mabao ya Azam FC katika mchezo wa leo yamefungwa na kiungo Idd Suleiman ‘Nado’ dakika ya pili akimalizia pasi ya Mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma na beki Mganda, Nicolas Wadada dakika ya 23 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa.


Bao pekee la Biashara United ya Mara leo limefungwa na mshambuliiaji wake hodari, Inocent Edwin dakika ya 35 na kwa kupoteza mechi hiyo timu hiyo inabaki nafasi ya 17 katika ligi ya timu 20 ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi 10.

Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, YANGA SC imeshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC 1-0 bao pekee nyota wa Rwanda Partrick Sibomana dakika ya 76 Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 

Post a Comment

0 Comments