BETI NASI UTAJIRIKE

ALICHOSEMA MKWASA BAADA YA KUSHINDA MCHEZO WAKE WA KWANZA AKIWA NA YANGA

Klabu ya Yanga imetangaza kurudi kwenye mbio za ubingwa baada ya kushinda bao1-0 dhidi ya Ndanda FC mchezo uliopigwa dimba la Nangwanda na kushuhudia mshambuliaji 


hatari raia wa Rwanda Patrick Sibomana akiipa ushindi Yanga. Baada ya Mchezo huo Kocha wa Yanga Boniface Charles Mkwasa alisema  : 

"Namshukuru mwenyezi Mungu na vijana wangu wamefanya yale tuliyopanga pamoja na kwamba tulipata muda mfupi wa maandalizi lakini kwa asilimia kubwa tumeweza tekeleza mipango yetu na tunashukuru  , Mechi ilikuwa ni ngumu kwani Ndanda wanatimu nzuri ila sisi tulikuwa bora zaidi yao na tusubiri mechi zijazo "

Aliongeza 
"Mipango yetu ni kucheza mpira wa kushambulia na kuna wakati tunacheza mpira na hata tunaposhambuliwa basi hurudi wote kukaba . Hawa vijana wanakaza sana wanapocheza na Yanga na kama wangekuwa wanacheza hivi naamini wangekuwa kwenye nafasi nzuri sana. Bado hatujawa na watu maalumu wa kupiga faulo na penati, nimekaa na tmu kwa muda mfupi na nilikuwa naangalia wanavyocheza"

Post a Comment

0 Comments