BETI NASI UTAJIRIKE

ALICHOSEMA KOCHA WA TAIFA STARS BAADA YA KUWAFUNGA EQUATORIAL GUINEA

Kocha mkuu wa Taifa Bw.Etienne Ndayiragije amezungumzia ushindi walioupata dhidi ya Equatorial Guinea . Kocha huyo ameonekana kufurahia viwango vya wachezaji 



Kocha huyo ametembea kifua mbele baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa taifa.Magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Msuva dakika ya 68 na Sure Boy dakika ya 90 ya  mchezo huo 

Kocha mkuu Bw. Etienne amefunguka na kuzungumzia ushindi huo kwa kusema 

" tulihitaji sana hizi pointi za mwanzo kwa sababu ndiyo mwanzo kabisa wa kutafuta nafasi kurudi AFCON na tunashukuru Mungu kwani mipango tulikuwa nayo na Mungu akabariki, vijana wamepambana na sapoti ya nyumbani imesaidia na nashukuru kuona jinsi mashabiki waliwasha mpaka tochi na iliamsha ari ya wachezaji , na hata vyombo vya habari vimefanya kazi kubwa na nzuri. Wengi wenu mlitupa taarifa ya jinsi timu hiyo inavyocheza ,mlielezea jinsi Equatorial Guinea wanavyocheza na kwa pamoja tumefanikiwa kupata ushindi. Binafsi naita ni ushindi wa nchi"

Taifa Stars itasafiri kuelekea nchini Tunisia siku ya jumapili kukabiliana na Libya kwenye mchezo wa pili wa makundi na mechi hiyo itafanyika tarehe 19 Novemba

Post a Comment

0 Comments