YANGA YAJIPANGA KUMTWAA KIUNGO WA SIMBA

Klabu ya Yanga imeshaanza mipango ya usajii wa dirisha dogo na hatua hiyo imefikiwa baada ya timu hiyo kufungwa na Pyramids pamoja na Ruvu shooting  msimu huu. 


Yanga imekuwa na changamoto eneo la kiungo mshambuliaji hivyo imejipanga kufanya usajili wa maana.Taarifa za ndani zinasema kuwa aliyekuwa kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima kuna uwezekano mkubwa akarejea Yanga msimu wa dirisha dogo.

Niyonzima ambaye hivi sasa anakipiga katika klabu ya AS Kigali Rwanda ameingia katika rada za Yanga kwa ajili ya kuboresha safu ya kiungo ya timu hiyo.

Taarifa zinasema safu hiyo ndani ya Yanga imekuwa inayumba tangu kuondoka kwa Ibrahim Ajibu ambaye alikuwa na mabingwa hao wa kihistoria msimu uliopita.

Inaelezwa dili hilo lilianza kusukwa na Bin Kleb ambaye alikuwa nchini Rwanda ambapo Taifa Stars ilikuwa inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda.

Licha ya kuwepo kwa taarifa hizo, uongozi wa Yanga umegoma kuzungumzia lolote hivi sasa na badala yake wamesema kwa sasa wanajipanga kumalizana na Pyramids katika mechi ya maruadiano ya Kombe la Shirikisho huko ugenini.

Post a Comment

0 Comments