TETESI ZA SOKA ULAYA LEO TAREHE 16 MEI 2024

 Bayern Munich wana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes msimu huu wa joto na wanaamini kuwa wanaweza kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 kwa sababu ya hali ya kufadhaika Old Trafford. (Independent)

Wachezaji kadhaa wakuu wa Bayern Munich akiwemo mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 30, wanataka meneja Thomas Tuchel kubadili uamuzi wake wa kuondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga mwishoni mwa msimu huu. (Abendzeitung - kwa Kijerumani)

Manchester United wako tayari kutoa pauni milioni 55 kumnunua beki wa Everton na England chini ya umri wa miaka 21 Jarrad Branthwaite, 21. (Daily Mail).

Mlinzi wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, anaelekea kuondoka Beyer Leverkusen msimu huu wa joto huku Real Madrid, Manchester City, Arsenal na Manchester United zikiwa na nia ya kunufaika na kipengele cha pauni milioni 35 katika mkataba wake. (Bild - kwa Kijerumani - usajili unahitajika)

AC Milan wanamsaka beki mpya na beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 25 wa Brazil Emerson Royal yuko juu kwenye orodha yao ya wachezaji walioteuliwa. (Fabrizio Romano)

Manchester United wanamenyana na Newcastle United katika mbio za kumnunua beki wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26. (Talksport)

Liverpool wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Nice na Ufaransa Khephren Thuram, 23, kwa pauni milioni 13 msimu huu. (Mirror)

Mkufunzi wa Feyenoord Arne Slot anapanga kumfanya meneja wake msaidizi Sipke Hulshoff uteuzi wa kwanza wa wahudumu wake wa klabu ya Liverpool atakaporithi mikoba ya Jurgen Klopp. (ESPN)

Wolves wanatarajiwa kumpa meneja Gary O'Neil kandarasi mpya ya miaka mitatu. (i Sport - usajili unahitajika)


Post a Comment

0 Comments