advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA WAREJEA DAR KIMYA KIMYA

Klabu ya Yanga imerejea jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wake dhidi ya Zesco United huko ndola Zambia.

Zesco waliutumia vizuri uwanja wa nyumbani na kuwafanya wapinzani wao Yanga kurejea nyumbani vichwa chini.

Zesco waliibuka kidedea kwa jumla ya magoli 3-2 dhidi ya Yanga. Katika mchezo wa awali uliopigwa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na katika mchezo wa pili Yanga alitandikwa magoli 2-1 na Zesco mjini Ndola.

Mbali na matokeo hayo mabovu kwa Yanga bado imesalia kwenye mashindano ya Caf na sasa itacheza mtoano Kombe la Shirikisho na endapo itashinda mechi hiyo basi itaingia moja kwa moja hatua ya Makundi.

Kwa upande wa ligi kuu Tanzania bara ,Yanga inajiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania. Mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Ruvu shooting Yanga walipoteza mchezo kwa bao 1-0


Post a Comment

0 Comments