advertise with us

ADVERTISE HERE

YANGA WAMTELEKEZA MZEEE AKILIMALI

Mjumbe wa baraza la wazee klabu ya Yanga mzee akilimali amewalaumu viongozi wa klabu hiyo kumtenga.
Mzee huyo anasumbuliwa na mgonjwa wa kisukari kwa mwezi wa pili sasa huku klabu hiyo kuonekana kutomjali kwa popote.

Akilimali amedai kwa sasa haoni vizuri na amedhoofika sana kwa kukosa huduma stahiki huku viongozi wa Yanga wakimuacha bila msaada wowote.

Akilimali ameiambia amospoti.com kwamba alielekea klabuni hapo kwa bajaji na alikutana na moja ya viongozi wa juu lakini kiongozi hakuonyesha nia ya kumsaidia.

Mzee huyo alirejea nyumbani kwako maeneo ya tandale na kuomba klabu hiyo na mashabiki wake wamsaidie kwa hali na mali ili aweze kurejea kama hapo awali.

Post a Comment

0 Comments