MASTAA WATANO KUTOKA AFRIKA WALIOWAHI KUTIKISA LA LIGA

Wengi wa wachezaji wa kiafrika wamewika soka la ulaya ila leo www.amospoti.com imekuandalia orodha ya wachezaji watano waliofanya vizuri zaidi ligi kuu Hispania maarufu kama La Liga.


GEREMI NJITAP 

Mchezaji huyu raia wa Cameroon ameacha historia kubwa kwa klabu  ya  Real Madrid. Mchezaji huyu aliisaidia klabu hiyo kutwaa mara mbili Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)  Mchezaji huyu  alielekea Chelsea na alifanikiwa pia akiwa huko.

Kwa upande wa kimataifa ,mchezaji huyo aliisaidia Cameroon kutwaa kombe la AFCON mara mbili mwaka 2000 na 2002. Mchezaji huyo aliisaidia timu hiyo kutwaa medali ya dhahabu kwnye michuano ya OLYMPIC.

THOMAS NKONO 

Golikipa huyu raia wa Cameroun ameichezea Espanyol ya Hispania kwa miaka 10 mfululizo na alitwaa medali ya mchezaji bora wa Africa  mara mbili mfululizo. Mchezaji huyo ameisaidia Cameroon kutwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1985.


Nkono aliweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kutoka ukanda wa Africa ya kati kufungwa bao moja tu kwenye kombe la dunia wakati timu hiyo ilipoondolewa hatua ya makundi bila kufungwa mechi yoyote mwaka 1982.

MICHAEL ESSIEN 

Essien hajafanya maajabu yoyote ndani ya La Liga tangu aliposajiliwa na Real Madrid chini ya Mourinho. Mchezaji huyo alikuwa na uwezo wa hali ya juu lakini majeraha yaliharibu kipaji chake.


Essien alishawahi kutwaa tuzo ya BBC Best player of the year Africa na alishawahi twaa kombe la ligi ya mabingwa ulaya , EPL na FA akiwa Chelsea. Mwaka 2010 majeraha yalimkosesha mchezaji huyo kuitumikia Ghana iliyofika robo fainali

YAYA TOURE

Kiungo huyu raia wa Ivory Coast ilifanikiwa kuitumikia Barcelona kwa kiwano cha hali ya juu na alisaidia upatikanaji wa makombe mawili ya La Liga na Champions Ligi mwaka 2009 dhidi ya Manchester United mchezo uliomalizika kwa Barcelona kushinda mabao 2-0 na Yaya Toure akifunga bao la kwanza.

Toure alijiunga na Manchester City mwaka 2009 na ni moja ya wachezaji walioijenga klabu hiyo kwa upya akishinda makombe matatu likiwamo kombe la FA. Mchezaji huyo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji bora wa Afrika mara nne mfululizo.

SAMUEL ETO'O 

Mshambuliaji hatari zaidi kwa Afrika karne ya 21 akiwwa ameshinda tuzo ya mchezaji bora Africa mara 4 sawa na Yaya Toure. Mchezaji huyo ameichezea klabu ya Real Madrid,Real Mallorca na Barcelona kwa miaka mitano. Mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora  zaidi wa klabu ya Real Mallorca .


Mchezaji huyo amecheza michezo 144 ya La Liga akifunga mabao 108 na ameisaidia Barcelona kutwaa Champions League mara mbili (2009 na 2009)

Akiwa na Cameroon Eto'o ameisaidia timu hiyo kutwaa tuzo makombe mawili ya AFCON  akiwa mfungaji bora wa mwaka 2006 na 2008 . Eto'o ameisaidia Cameroon kutwaa medali ya Dhahabu Olumpic na ameiongoza timu hiyo kucheza kombe la dunia mara tatu mfululizo.

Post a Comment

0 Comments