UFAHAMU UWANJA WA PYRAMIDS UTAKAOTUMIWA DHIDI YA YANGA

Kuelekea mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho kati ya Pyramids na Yanga nimekuandalia makala maalumu kuhusiana na  timu ya Pyramids itakayoikaribisha Yanga nchini Misri.



Mchezo huo wa marudiano utapigwa  tarehe 03 Novemba 2019 kwenye uwanja wa nyumbani wa Pyramids uitwao 30 June  Stadium.

HISTORIA FUPI YA UWANJA .

Uwanja wa 30 June Stadium ulijengwa na unamilikiwa na jeshi la anga la Misri. Uwanja huu hutumika kwa michezo mbalimbali ikiwamo Mpira wa miguu na michezo ya kukimbia. Uwanja upo jijini Cairo na unauwezo wa kujaza mashabiki 30,000. Uwanja huu hutumiwa na klabu ya Pyramids kwenye michezo ya ligi kuu Misri na mashindano mbalimbali ya kimataifa.


MAJANGA YALIYOWAHI KUTOKEA 

Tarehe 8 february 2015 uwanja huu ulisababisha vifo vya watu 22. Ilikuwa ni mechi kati ya Zamalek na Ennpi . uwanja huo ulikuwa umejaa sana hivyo iliwalazimu polisi kuzuia mashabiki kuingia uwanjani hapo ndipo fujo zilipoanza na Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya , kitendo hicho kilizua majanga zaidi kwani mashabiki hao walikanyagana na watu 22 walipoteza maisha.

ZAHERA , WACHEZAJI WA TAIFA STARS WANAUFAHAMU HUU UWANJA 

Uwanja huo si mpya kwa Kocha Zahera kwani aliutumia uwanja huu kuwaadhibu Zimbabwe mabao 4-0 dhidi ya Congo kwenye mchezo wa AFCON 2019. Uwanja huu haukuwa na bahati nzuri kwa akina Fei Toto,Kelvin Yondani  na timu ya taifa "Taifa Stars kwani walifungwa mechi zote mbili ikiwamo Mechi ya Senegal vs Taifa Stars (2-0) na ule wa Kenya vs Taif Stars (3-2).

Tutazidi kukusogezea kila habari ihusuyo mechi kati ya Yanga vs Pyramids

Post a Comment

0 Comments