advertise with us

ADVERTISE HERE

TAJIRI WA YANGA NOMA ,ATANGAZA KUMWAGA PESA KUMZIDI MO DEWJI

Baada ya kupewa milioni 10 jana ambazo zilikuwa kama sehemu ya hamasa ili kushinda mechi ya ligi dhidi ya Coastal Union.
 lengo ambalo lilifanikiwa, inaelezwa kuwa Kampuni ya GSM itaendelea na mpango wa kuendelea na ahadi ili kutoa nguvu kwa wachezaji.

Taarifa za ndani zinasemea mpango huo unafanywa na mabosi wa Yanga ili kusaidia timu iweze kupata matokeo baada ya kufanikisha hilo kwenye mechi ya jana dhidi ya Coastal Union ambayo walishinda bao 1-0.

Yanga ambao wanadhaminiwa na GSM wanaweza wakawa wamefunguliwa neema ya kuendelea kupokea mamilioni zaidi wakizidi kufanya vema.

Fedha hizo zitaendelea kuwa sehemu ya motisha kwa wachezaji kuzidi kujituma na kufanya vema ili kurejesha morali ya kuwania taji la ligi msimu huu.

Post a Comment

0 Comments