SIMBA YAPOTEZA MCHEZO WA LIGI KUU KWA MARA YA KWANZA

Klabu ya Simba SC imejikuta ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mwadui kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania. Mchezo huo ulichezwa dimba la CCM Kambarage


Mkoani Shinyanga .Simba imepoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu. Kabla ya mchezo huo ilikuwa  imecheza michezo 6 na kupata pointi 18 pasipo  kupata sare wala kufungwa.

Goli la Mwadui lilifungwa na Gerald Mathias dakika ya 33 na lilidumu mpaka dakika ya 90. Simba ilionyesha uwezo wa hali ya juu kwenye mchezo huo ikimiliki mpira kwa asilimia 56 dhidi ya 44.Ilipiga jumla ya mashuti 7 huku mashuti 3 yakilenga golini huku mwadui wakipiga mashuti 4 na mawili kulenga golini na moja kuzaa bao hilo pekee.Mwadui imepanda mpaka nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania.

Matokeo mengine ni Ruvu Shooting 1 vs  0 KMC, Mtibwa Sugar 2 vs 1 Coastal Union, 
 Lipuli 2 vs 1Polisi Tanzania,  Kagera 2 vs 0 Namungo, Singida 1 vs 2 JKT Tanzania.

Post a Comment

0 Comments