SIMBA KUENDELEA KUTOA KICHAPO KWA MWADUI

Washambuliaji tegemezi  wa Simba Meddie Kagere na Miraji Athumani wataiongoza timu hiyo kuisambaratisha Mwadui  kwenye mchezo wa ligi kuu Vodacom .


 Mchezo huo utaanza saa 10 jioni kwenye uwanja wa kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.  Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo wowote tangu ligi ianze.

 Simba imecheza mechi 6 na kushinda zote hivyo kujikusanyia pointi 18 na wafungaji wake Meddie Kagere akifunga mabao 7 na Miraji Athuman akifunga mabao 4.

Mshambuliaji John Bocco ataendelea kukosekana kwenye mchezo huo kutokana na majeraha aliyoyapata sambamba na beki kisiki Tshabalala ambaye ameanza mazoezi mepesi.

Mwadui wameanza vibaya ligi kuu Tanzania baada ya kuruhusu mabao 7 kwenye mechi 8 za ligi kuu. Mwadui imeshinda mchezo mmoja tu ikitoa sare 5 na kufungwa mechi 2 hivyo kushika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu Vodacom.

Post a Comment

0 Comments