ads

adds

CRISTIANO RONALDO AKABIDHIWA UWANJA BAADA YA KUFUNGA GOLI LA 700

Mchezaji wa Juventus na timu ya taifa Ureno Cristiano ameendelea kuweka rekodi mpya kila kukicha baada ya hapo juzi kufunga goli lake la 700 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.


Mara baada ya goli hilo klabu yake ya zamani iliyomkuza ya Sporting Libon ilisema uwanja wake utaitwa Cristiano Ronaldo kama ishara ya kumuenzi na kudumisha ukubwa wake katika soka.

Ronaldo alifunga goli hilo kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya timu za taifa ulaya EURO 2020 dhidi ya Luxemboug na kumfanya aendelee kushikilia rekodi ya mabao mengi zaidi kwa wachezaji wanaocheza soka kwa sasa.

Mbali na uwanja huo kupewa jina lake lakini pia mwaka 2017 uwanja mmoja wa ndege  nchini Ureno ulipewa jina la Cristiano Ronaldo International Airport.

Ronaldo amekuwa ni msaada n nembo ya taifa la Ureno kwenye medani za soka baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa makombe matatu ya ulaya ikiwamo EURO 2, NA UEFA NATIONAL LEAGUE 1. ndiye mchezaji mwenye magoli mengi zaidi kwa timu yake ya taifa na anashikiria tuzo 5 za mchezaji bora wa dunia kwa ukanda wa ulaya.

Post a Comment

0 Comments