advertise with us

ADVERTISE HERE

PYRAMIDS FC YAJIBU FIGISU ZA YANGA KWA KISHINDO

 Mabosi wa Pyramids FC ya Misri wameahidi donge nene kwa wachezaji wao endapo wataitoa Yanga kunako Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga na waarabu hao watakutana katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza itakayokuwa ni ya kuwania kufuzu hatua ya makundi.

Taarifa zinasema mabosi wa waarabu hao wameahidi donge hilo kama sehemu ya motisha ili timu hiyo itinge hatua ya makundi ndani ya mashindano hayo.

Timu hiyo inayotajwa kufanya usajili wa mabilioni, mpaka sasa ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wa Misri ikiwa na alama 7 baada ya kucheza mechi tatu ikishinda mbili na mmoja ikienda sare.

Post a Comment

0 Comments