Taarifa isiiyokuwa rasmi inasemaa wachezaji wa Lipuli wanashikiliwa na jeshi la Polisi Iringa.Inadaiwa wachezaji hao wamewekwa chini ya ulinzi na hakuna sababu iliyoelezwa.
Kupitia idara ya Habari na Mahusiano timu hiyo imetoa taarifa hiyo tarehe 29/10/2019.Taarifa hiyo imenukuliwa ikisema
"Uongozi wa Lipuli unasikitika kuona Jeshi la Polisi limewakamata wachezaji wetu 4 akiwemo Paul Nonga, Issa Ngoah, Seif Karihe na Daruwesh Saliboko.
Wachezaji hao wamepigwa na kuchaniwa nguo na kuwapeleke kituo cha Polisi
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa moja jioni wakati wachezaji wetu kwa pamoja wakitoka katika ofisi za klabu zilizopo nje ya uwanja wa Samora."
Baadhi ya viongozi wa klabu wapo kituo cha Polisi kujaribu kufatilia kwa karibu jambo hili. Amospoti.com inafuatilia tukio hilo kwa umakini na italitolea taarifa zaidi .
0 Comments