Klabu ya Simba imeendelea kufanya vizuri kwenye michezo yake ligi kuu Tanzania bara baada ya kushinda michezo yake yote 4 iliyocheza na kujikusanyia pointi 12.
Mbali na ushindi huo. Simba imeweka rekodi ya kushinda magoli 13 ikiwa imefungwa magoli 2 pekee. Simba haikuishia hapo tu kwani mshambuliaji wake mahili Meddie Kagere ameweza kufunga mabao 6 kwenye michezo minne aliyocheza.
Simba inampango mahususi wa kushinda vikombe vyote inavyoshiriki msimu huu na hii imejidhihirisha baada ya kutofungwa mechi yoyote tangu ilipofungwa na TP-Mazembe kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita
Uwepo wa Kagere umeendelea kuimarisha safu ya ushambuliaji Simba na wapinzani wamekuwa wakiihofia timu hiyo.
0 Comments