BETI NASI UTAJIRIKE

MWISHO WA KELVIN YONDANI UMEFIKA ?

Beki mahili wa Yanga na Taifa Stars amewashangaza mashabiki wa klabu na wapenzi wa soka nchini baada ya kumweka wazi mrithi wa nafasi yake ndani ya kikosi cha Taifa Stars.


 Yondani anaamini beki wa Coastal Union Bakari Mwambyeto ndiye anauwezo wa kuziba nafasi yake iwapo atastaafu kuichezea timu ya taifa Taifa Stars.

Yondani ametoa kauli hiyo kufuatia beki huyo kuonyesha kiwango kizuri katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (Chan) dhidi ya Sudan ambao Stars imefuzu kwa faida ya bao la ugenini.

Yondani alisema kuwa anaamini beki huyo ana uwezo mkubwa wa kuchukua mikoba yake ndani ya kikosi hicho kutokana na kucheza kwa utulivu mkubwa pamoja na kutumia akili ya kupambana na washambuliaji kama ilivyokuwa kwa upande wake.

“Binafsi naona yule Mwamnyeto anaweza kucheza kwenye nafasi yangu vizuri katika kikosi cha timu ya taifa, kwa sababu amekuwa akicheza kwa utulivu mkubwa na anajua vizuri kupambana na washambuliaji.

“Naamini atakuwa msaada maana uchezaji wake hautofautiani na mimi, mara kadhaa nimekuwa nikimpigia simu kumueleza hilo kwa sababu navutiwa na uchezaji wake na hata kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Chan dhidi ya Sudan ubora wake umeonekana,” alisema Yondani.

Post a Comment

0 Comments