advertise with us

ADVERTISE HERE

MOLINGA ATANGAZA VITA KWA WAARABU

Straika wa Yanga, David Molinga, amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kutokuwa na hofu kuelekea mechi yao na Pyramids FC ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itakuwa na kibarua cha raundi ya kwanza ya michuano hiyo jijini Mwanza kwenye dimba la CCM Kirumba dhidi ya waarabu hao wa Misri.

Taarifa imeeleza Molinga ama Falcao, ameeleza kuwa wao kama wachezaji wanazidi kujipanga kwa ajili ya kuwaonesha kazi waarabu.

Amesema wanajua namna gani mashabiki na wanachama wanavyotegema matunda kutoka kwao, naye kama mchezaji ameeleza kuwa watapambana ili wasipoteze.

Baada ya mechi hiyo, Yanga itasafiri kuelekea Misri kucheza mchezo wa marudiano utakaopigwa Novemba 03 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments