ads

adds

MKUDE APEWA ONYO KALI NA SIMBA

Taarifa za ndani kutoka kwa CEO mpya wa klabu ya Simba, Senzo Mazingiza amemtaka kiungo wa klabu ya Simba,


Jonas Mkude anatuhumiwa kunywa pombe. Mazingiza amemtaka Mkude kuacha tabia hiyo akiwa kambini au wanapopewa mapumziko ya muda mfupi.

Ikumbukwe Mkude aliachwa kwenye msafara wa timu ya Simba ulioenda Kanda ya Ziwa kwa madai ya kwamba alipitiwa na usingizi akachelewa kuamka na amekiri kosa na kuomba msamaha.

Hii si mara ya kwanza kwa Mkude kuachwa nje ya kikosi kutokana na utovu wa nidhamu, na ikumbukwe aliwahi kuvuliwa ukapteni sababu ya matukio kama haya miaka kadhaa huko nyuma.

Aidha, Mkude pia aliwahi kuachwa hivi karibuni katika moja ya safari ambayo ilikuwa ni kuelekea mkoani kwa ajili ya mechi za ligi baada ya kuchelewa ndege Airport.

Post a Comment

0 Comments