ads

adds

MIRAJI ATHMANI ANAVYOUTAFUTA UFALME KIMYA KIMYA PALE SIMBA

Mchezaji wa Klabu ya Simba Sc ameanza kuwa kivutio kwa wachezaji na mashabiki  wa klabu hiyo baada ya kufanya mambo makubwa na kushangaza msimu huu.
Mchezaji huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba baada ya kufunga mabao mawili huku akitengeneza mengine mawili na kumfanya awe na mchango wa mabao 4 kati ya 10 yaliyofungwa na klabu hiyo.

Mara baada ya kuchaguliwa uchezaji bora kwa mwezi Septemba mchezaji huyo alikabidhiwa kiasi cha shilingi milioni 1 na kisha aliamua kuzigawa kwa kila mchezaji wa klabu hiyo kama shukrani kwa mchango wao.

Je anajengaje ufalme wake ?

Msimu huu Miraji Athmani ameuanza vyema kwa kuchangia upatikanaji wa mabao manne huku kwenye orodha ya wafungaji bora ligi kuu akishika nafasi ya pili nyuma ya mchezaji mwenzake wa Simba Meddie Kagere m,wenye goli 6.

Vyombo vya habari , mashabiki na wachambuzi walianza kulitaja jina la Miraji Athmani na kumfanya afahamike kwa haraka . Kwa upande mwingine kitendo cha kugawanya fedha aliyopata kwa wachezaji wenzake kinatia motisha na jina lake litazidi kusambaa kwa urahisi. Mbali na hayo Miraji anapambania nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha kwanza na kama akifanikiwa basi ndoto zake zitatimia.

Post a Comment

0 Comments