MESSI ATANGAZA KURUDI RASMI LA LIGA BARCELONA WAKISHINDA 5-1

Mchezaji bora wa dunia Lionel Messi ameendelea kuonyesha ubora wake baada ya hapo jana kufunga mabao mawili dhidi ya Valladolid mchezo wa La Liga.


Mshambuliaji huyo alianza msimu huu akiwa majeruhi na alilazimika kukosa baadhi ya mechi. Lionel Messi amerejea rasmi La Liga na kufunga mabao mawili huku akichangia upatikanaji wa bao 1.

 Mchezo huo ulipigwa dimba la Nou Camp na Barcelona walipata bao la kuongoza kupitia kwa beki wake wa kati Clement Lenglet dakika ya 2 ,Vidal alifunga bao la pili dakika ya 29 , Lionel Messi alifunga mabao dakika ya 35 na 75 huku Suarez akimalizia bao la tano dakika ya 77.

Kwa matokeo hayo Barcelona imeendelea kukaa kileleni kwa pointi 22 kwenye mechi 10 walizocheza wakifuatiwa na Granada na Atletico zenye pointi 20 na zimekwishacheza michezo 10 kila moja. Real Madrid anapointi 18 na mchezo mmoja mkononii dhidi ya Leganes mhezo utakaopigwa dimba la Santiago Bernabeu. Kama Real Madrid watashinda mchezo huo basi basi watashika nafasi ya 2 nyuma ya Barcelona  kwa tofauti ya pointi 1


Post a Comment

0 Comments