advertise with us

ADVERTISE HERE

MBRAZIL WA SIMBA ASHINDWA KUONYESHA UWEZO WAKE DHIDI YA BANDARI

Mshambuliaji Mbrazil Wilker Da Silva wa Simba aliesajiliwa msimu huu ameshindwa kuonyesha cheche zake kwenye mchezo wa kiafiki dhidi ya Bandari kutoka Kenya.Mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja tangu msimu unaanza kwa kusumbuliwa na majeraha . Hapo Jana kocha Patrick Ausen alimuanzisha mshambuliaji huyo kwenye mechi na Bandari na kuptia mchezo huo Da Silva alipiga shuti moja kwa kipindi cha dakika 45.

Simba walipata kona 3 na zote ziliokolewa na mabeki wa bandari na hazikuwa na madhara yoyote.Da Silva alionekana kuzunguka uwanjani bila kufanya kitu cha ziada ambacho kingepelekea mashabiki wa Simba kumfurahia.

Kutokana na kusindwa kuonyesha uwezo kwenye mechi hii Simba itaendelea kuwategemea zaidi John Boko na Meddie Kagere kwenye safu ya ushambuliaji.

Post a Comment

0 Comments