Tarehe 31 Oktoba 1997 alizaliwa nyota mahili wa Manchester United Marcos Rashford. Nyota huyo ameendelea kuwa habari ya mjini baada ya hapo jana kufunga mabao mawili
Dhidi ya chelsea kwenye mchezo wa mtoano kombe la ligi (carabao cup) uliomalizika kwa manchester kushinda mabao 2-1 na Manchester kucheza robo fainali .
Goli lake la pili alipiga kwa staili ya Cristiano Ronaldo na kila mtu alishangazwa kwa umahili wake.
Nyota huyo anatimiza miaka 22 na amekuwa na magoli 52 tangu aanze kutumikia kikosi cha kwanza cha Manchester United akitokea akademia ya timu hiyo. Rashford anacheza kikosi cha kwanza timu ya taifa Uingereza tangu mwaka 2016.
Rashford anajiingizia Paundi million 10 kwa mwaka kupitia mshahara na mikataba mbali mbali na amekuwa akifananishwa kama Ronaldo mpya wa Manchester United .
0 Comments