advertise with us

ADVERTISE HERE

MANULA KUENDELEA KUIKOSA TAIFA STAZI SABABU ZATAJWA

Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amefunguka kuhusiana na kuendelea kumuacha kipa wa Simba, Aishi Manula katika kikosi cha Taifa Stars.


Ndayiragije ameeleza kuwa Manula alimuomba mwenyewe kuwa anaomba akapumzike sababu aliumia mara baada ya kumuita wakati wanaenda kucheza mechi ya kuwania kufuzu CHAN dhidi ya Kenya.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Burundi, amesema kinachotakiwa kwa Manula ni kuonesha kiwango kizuri akiwa ndani ya klabu yake na akiona anafaa tena atamuita sababu ametoka majeruhi siku si nyingi zilizopita.

Aidha, Ndayiragije amefunguka kwa kusema kuwa Stars si timu ya mtu mmoja kwani kila kila mchezaji ana nafasi ya kuitumikia timu hiyo maana ni ya watanzania wote.

Post a Comment

0 Comments