MANCHESTER UNITED YAENDELEZA UBABE KWA CHELSEA

Klabu ya Manchester United inaonekana imezinduka toka usingizini na sasa haitaki utani kwa timu yoyote inayokutana nayo. Manchester United ilianza ligi kuu


 Kwa kusuasua na kwa sasa imeonekana kurejea kwenye fomu na kuimarika zaidi. Klabu hiyo ilionekana kurejea kwenye kiwango kizuri baada ya kupata sare na timu ngumu ya Liverpool kisha kushinda mabao 3-1 dhidi ya Norwich na hapo jana imeitandika Chelsea mabao 2-1 kwenye kombe la Ligi.

Historia fupi kati ya Chelsea vs Manchester United 

Tangu msimu wa 2018/19 mpaka sasa timu hizo zimecheza michezo 7 huku Manchester United ikishinda michezo 4  Sare 2 na huku ikipoteza mchezo mmoja tu kwa Chelsea.

Msimu wa 2019/20 Chelsea na Manchester United zimekutana mara mbili na Manchester United imeibuka na ushindi wa mechi zote mbili ikishinda mabao 4-0 Ligi kuu na 2-1 Carabao Cup. Matokeo hayo yanaifanya United kuonekana bora zaidi msimu huu na kuendeleza ubabe wake.

Marcos Rashford aliibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga mabao 2 peke yake na kuipeleka timu hiyo robo fainali Carabao Cup.

Post a Comment

0 Comments