Lukaku alinunuliw na Jose Mourinho mwaka 2017 na alicheza michezo 66 akifunga mabao 28 tu. Mshambuliaji uyo alishindwa kuendana na staili ya Ole Gunnar na msimu wa majira joto aliuzwa kwenda Intermilan ya Italy.
Akiwa Intermilan amecheza mechi 9 na kufunga mabao 6 huo ni mwenendo mzuri kwa mchezaji huyo. Lukaku ameichezea timu yake ya taifa Belgium kwa mafanikio makubwa akifunga mabao 51 kwenye mechi 83. Lukaku anaumri wa miaka 26 na anazidi kuwa imara zaidi.
Kwa upande wa Manchester United wamejikuta katika matatizo kila kukicha kutokana na kukosekana kwa mshambuliaji wa uhakika.Klabu hiyo inawategemea makinda wake James,Rashford na Martial ambao wote wamekuwa wakipata majeraha ya mara kwa mara. Klabu hiyo imefunga mabao 13 na kufungwa mabao 10 huku ikishinda mechi 3 sare 4 na kufungwa mechi 3. Matokeo hayo yanaifanya manchester united kuwa na pointi 13 ikiwa nafasi ya 7 ikipishana na Liverpool inayoongoza ligi kwa pointi 15.
Lukaku ameiwezesha Inter milan kuongoza ligi kuu Italy "Serie A" kwa kuipa timu hiyo bao la ushindi alilofunga dakika ya 63 dhidi ya Brescia.
Mashabiki wa manchester united wamekuwa wakijilaumu kumuuza mchezaji huyo kwani alihitajika zaidi msimu huu kutokana na anavyocheza.
0 Comments