BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER CITY YAENDELEZA UBABE KWA TIMU ZA UINGEREZA

Klabu ya Manchester City imeendelea kutoshikika  baada ya kuifunga Southampton kwa mabao 3-1 kwenye mchezo hatua ya mtoano kombe la Carabao. 


Manchester City imefuzu robo fainali na mshambuliaji wake hatari Kun Aguero akindelea kuadhibu timu pinzani zinazokutana na timu hiyo. kwenye mechi hiyo Aguero alifunga mabao 2 na  bao la tatu likifungwa na Otamendi. Manchester City inaendelea kulitetea kombe la Carabao ililoshinda msimu wa 2018/19.


Gumzo ni pale klabu  ngeni za  Oxford United na Colchester United kuingia robo fainali baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo yao ya jana usiku.Michuano hiyo inaendelea tena leo usiku na itazikutanisha Chelsea Arsenal Liverpool ,Manchester United,Aston vila na Wolves.



michezo inayosubiriwa kwa hamu ni ule wa,Chelsea ikiikaribisha Manchester  United na Liverpool ikiikaribisha  Arsenal huku Aston Villa ikiikaribisha Wolves.

Post a Comment

0 Comments