advertise with us

ADVERTISE HERE

MANARA AENDELEA KUWASAKAMA YANGA

Msemaji wa klabu ya Simba ameendelea kuwa mwiba mkali wa klabu hiyo baada ya kusema ni lazima awepo Mwanza siku ambayo Yanga itacheza na Pyramid.Manara ameutumia mtandao wa Instagram kutangaza vita na mashabiki wa Yanga na aliandika hivi "

"Guys nimealikwa tarehe hyo kuwa Mgeni rasmi ktk Graduation ya shule moja ya sekondari,So msije mkasema nimewafuata nyie,nakuja Mwanza na yangu!! Ila Gongowazi bana,nani kawaambia Israel unaweza kumkimbia? njia ya kuwakwepa Mafarao ni kujitoa tu"

Amewaambia Yanga hata kama wamekimbilia Mwanza ni lazima wafungwe na klabu ya Pyramid na yeye takuwepo Mwanza siku iyo ya mechi .

Mashabiki wa Simba wameonekana kumuunga mkono msemaji huyo na wamejipanga kwenda jijini Mwanza wakitokea Dar es Salaam. 

Baadhi ya matawi ya Simba ukanda wa ziwa yameonyesha dhahiri kuisapoti Pyramid FC itakayocheza na Yanga siku hiyo.

Post a Comment

0 Comments