advertise with us

ADVERTISE HERE

KWA YANGA HII WAARABU WAJIPANGE HASWAAA

Hayawi hayawi na sasa yamekuwa baada ya CAF kutoa ratiba mbali mbali  za mechi ngazi ya vilabu.


Yanga imepangwa na klabu inayoshiriki ligi kuu misri Pyramids fc. Klabu hiyo si maarufu sana kwa upande wa Africa lakini imekuwa ikifanya vyema ligi kuu misri na hata ligi ya mabingwa ulaya.

Mchezo wa kwanza utapigwa uwanja wa taifa jijini dar es salaam tarehe 27/10/2019 na mchezo wa pili utapigwa jijini Cairo mnamo tarehe 3/11/2019

Kwa kuanzia nyumbani Yanga inapaswa kutafuta magoli mengi ili iweze kufanya vizuri mchezo wa Marudiano.

Endapo yanga itafanikiwa kuitoa Pyramids basi itaingia hatua ya makundi kombe la shirikisho.

Timu za Uarabuni zimekuwa Chungu kucheza nazo hasa michuano hii. Kwa upande mwingine Yanga ni timu kongwe na inakikosi imara hivyo mchezo huo n lazima itashinda

Mwalim zahera anafaham hujuma za waarabu hivyo atamalizana na waarabu hapa hapa nyumbani na mchezo wa marudiano utakuwa mwepesi Kwake.

Post a Comment

0 Comments