KIONGOZI YANGA ASEMA NI MARUFUKU KUMLAUMU KOCHA ZAHERA

Mashabiki wa Yanga wameonekana kukasirishwa na usajili walioufanya mwaka huu kupitia  Kocha Mwinyi zahera. Lakini ukweli ni kuwa Zahera hapaswi kulaumiwa 




alisema moja ya viongozi wa zamani  wa klabu hiyo Mzee Abdul Sauko mzee huyo aliombwa atoe maoni yake kuhusiana na mwenendo wa Yanga hasa kwenye suala la usajili naye alinukuliwa akisema. 
 Mzee Abdul Sauko
"Kocha alitoa mapendekezo, na mapendekezo yale alipeleka kwa viongozi, viongozi walitakiwa wamuulize mwalimu (Mwinyi Zahera) hawa wachezaji unaowapendekeza ni wazuri kuliko hawa waliopo?
Kwa sababu ameondoka Ajibu, ameondoka Makambo, ameondoka Tambwe, nani aliyekuja ambaye anawazidi wale walioondoka? Utaratibu ni kwamba anayekuja awe na uwezo kama yule aliyeoondoka au amzidi yule aliyeoondoka.
Sasa Yanga walisajili watu bila kuangalia, wamekwenda tu wakachukua watu wakawajaza pale ndio maana unaona viongozi walitakiwa wamuulize mwalimu hawa wana uwezo?
Viongozi walikuwa na jukumu la kukaa chini na mwalimu na kujadili na kuwaambia wanasajili mastraika gani wa kufiti kwenye klabu ya Yanga, kitu hicho hakikufanyika.
Leo wakianza kusema kwamba kosa ni la Zahera sio kweli, kosa ni la viongozi pamoja na Zahera aliyependekeza lakini walikuwa na uwezo wa kumuuliza je hawa wachezaji wana uwezo?
Yanga inajianda na safari na wataondoka siku ya kesho tarehe 31/10/2019 kuelekea Nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Pyramids. Yanga inatakiwa kufunga mabao 2-0 au 3-1 ili iweze kufuzu hatua ya makundi.

Post a Comment

0 Comments